Posts

Showing posts from August, 2023

KITUO KIKUBWA CHA TAIFA CHA UBUNIFU KUJENGWA DAR

Image
Na Richard Mwaikenda, Dodoma TUME ya Tehama imeanzisha mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha Taifa cha Ubunifu Dar Es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma kwa wataalam, watafiti, na wabunifu wa TEHAMA. Mafanikio hayo na mengine lukuki ya Tume hiyo, yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume, Nkundwe Mwasaga (picha I) wakati wa mkutano wa na vyombo vya habari wa kuelezea utekelezaji wa majukumu  yao  kwa mwaka 2022/2023 na vipaumbele vyao kwa mwaka 2023/2024 kwenye Ukumbi Wa Idara ya Habari -MAELEZO, jijini Dodoma Agosti 25,2023. Mwasaga ametaja mafanikio mengine kuwa ni; # Kuanzisha kituo kimoja cha ubunifu TEHAMA (Softcentre) Zanzibar, vinne vya Kanda katika majiji ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Lindi na Mbeya kwa ajili ya kuendeleza kampuni changa za TEHAMA na kuendeleza kituo cha Dar es Salaam ili kukuza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa za TEHAMA na kukuza uchumi wa nchi. # Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT refurbishment and assembly centre). # ...