KITUO KIKUBWA CHA TAIFA CHA UBUNIFU KUJENGWA DAR
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
TUME ya Tehama imeanzisha mradi wa ujenzi wa kituo kikubwa cha Taifa cha Ubunifu Dar Es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma kwa wataalam, watafiti, na wabunifu wa TEHAMA.
Mafanikio hayo na mengine lukuki ya Tume hiyo, yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume, Nkundwe Mwasaga (picha I) wakati wa mkutano wa na vyombo vya habari wa kuelezea utekelezaji wa majukumu yao kwa mwaka 2022/2023 na vipaumbele vyao kwa mwaka 2023/2024 kwenye Ukumbi Wa Idara ya Habari -MAELEZO, jijini Dodoma Agosti 25,2023.
Mwasaga ametaja mafanikio mengine kuwa ni;
# Kuanzisha kituo kimoja cha ubunifu TEHAMA (Softcentre) Zanzibar, vinne vya Kanda katika majiji ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Lindi na Mbeya kwa ajili ya kuendeleza kampuni changa za TEHAMA na kuendeleza kituo cha Dar es Salaam ili kukuza kiwango cha uzalishaji wa bidhaa za TEHAMA na kukuza uchumi wa nchi.
# Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT refurbishment and assembly centre).
# Kuwezesha mafunzo maalum ya TEHAMA kwa wataalam kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.
# Kuwezesha mijadala miwili (2) ya wadau kutoka sekta ya Umma na Binafsi inayohusu maboresho ya sheria katika sekta ya TEHAMA na kuvutia uwekezaji ili kuharakisha ukuaji wa sekta kwa kuihusisha sekta binafsi.
# Mijadala ya TEHAMA na Sekta binafsi imeiwezesha Tume kusaini mikataba ya maelewano ya uwezeshaji katika TEHAMA na mashirikika na taasisi mbalimbali zikiwemo Benki ya CRDB, UNCDF, UNDP, DOT na UNESCO.
# Kutengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu TEHAMA nchini (ICT human capital development system): lengo la mfumo huu ni kutambua bunifu na kupanua wigo wa ukuzaji wa wabunifu na bidhaa na huduma za TEHAMA zinazozalishwa Tanzania na hivyo kukuza pato la Taifa na kuongeza fursa za ajira kupitia TEHAMA na maendeleo ya kidijitali duniani.
# Kuandaa mkutano wa mwaka wa TEHAMA (TAIC) na Tuzo ya TEHAMA Tanzania (Tanzania ICT Award): Hili lilikuwa kongamano kubwa la mwaka la TEHAMA lililofanyika Zanzibar mwezi Oktoba, 2022 na kuwashirikisha wawekezaji na wadau mbalimbali wa TEHAMA kutoka ndani na nje ya nchi wapatao 1,200.
# Kuendelea kusajili wataalam wa TEHAMA na kufikia 1,600 hadi tarehe 31 Juni, 2023.
VIPAUMBELE VYA TUME KWA MWAKA 2023/2024
▫️Kuendelea na ukamilishwaji wa vituo vya ubunifu TEHAMA (Soft centers) katika Kanda 5 pamoja na kuanzisha kituo kimoja Zanzibar.
▫️Kuanzisha kituo cha kutengeneza na kuboresha vifaa vya TEHAMA (ICT Refurbishment and Assembly centre).
▫️Kuwezesha uanzishaji wa vituo vya majaribio vya ubunifu TEHAMA (District ICT Startups Innovation hubs) katika Wilaya 10.
▫️Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA nchini na kufanya tathmini ya kitaifa ya hatua za utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya TEHAMA.
▫️Kuratibu na kuandaa matukio ya kuvutia uwekezaji na kutangaza masoko ya bidhaa za TEHAMA ndani na nje ya nchi.
▫️Kushirikiana na washirika wa maendeleo na kampuni za kimataifa katika kuendeleza bunifu za TEHAMA ikiwemo kuwezesha utengenezaji wa bidhaa za TEHAMA hapa nchini.
▫️Kujenga kituo cha Artificial Intelligence kwa ajili ya kuendeleza wataalam wa TEHAMA.
▫️Kuwezesha mafunzo maalum ya wataalam wa TEHAMA 500 ili kukuza na kuendeleza ujuzi wa TEHAMA nchini.
▫️Kukuza soko la bidhaa na huduma za kampuni ndogondogo “startup” kwa kushiriki maonesho na makongamano yanayohusu fursa za startups duniani.
▫️Kuratibu na kutengeneza mfumo wa usimamizi wa utekelezaji wa Sera ya TEHAMA na kufanya tafiti za kuweza kufanya maboresho ya sera kulingana na mabadiliko ya teknolojia.
▫️Kujenga metaverse studio kwa ajili ya kutengeneza maudhui ya metaverse na pia kuboresha maudhui ya mitandao.
▫️Kufanya tafiti za maendeleo ya TEHAMA kwa kila wilaya.
▫️Kuanzisha Kituo cha Resilience Academy hapa nchini.
Aliyosema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
# Serikali imeamua kuwekeza kwa nguvu kwenye Tanzania ya Kidijitali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo msimamizi mkuu unafanywa na Tume ya TEHAMA.
# Hili ni jambo kubwa kwani fedha nyingi imewekezwa kwa ajili ya kuboresha TEHAMA nchini kwani shughuli mbalimbali kwa sasa duniani zinafanyika kwa njia ya kidijitali ikiwemo huduma za malipo mabalimbali, huduma za afya za matibabu, uzalishaji, kilimo, uchimbaji wa madini.

Comments
Post a Comment